SIMBA KUSAKA USHINDI MWINGINE KWA LIPULI LEO
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu Bara Simba Sc jioni ya leo wanakuwa wageni wa Lipuli Fc katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Samora mjini Iringa.
Kwa hakika Simba leo inahitaji ushindi mwingine muhimu ili kujiwekea matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuhangaika kipindi cha miaka mitano bila mafanikio.
Lipuli inayonolewa na kiungo wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Seleman Matola ambaye inaonekana pia ameongezewa nguvu na kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula "Mzazi" kwa vyovyote wanataka kuizuia Simba yenye safu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya