Okwi bado hajavunja rekodi ya Tambwe

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Sc, Mganda, Emmanuel Okwi kwa sasa ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoendelea akiwa amepachika magoli 19.

Okwi anafuatiwa na John Bocco "Adebayor" mwenye magoli 14 na Obrey Chirwa mwenye mabao 12, Adebayor ni mchezaji wa Simba wakati Chirwa ni wa Yanga.

Lakini tayari Okwi ameshavunja rekodi za baadhi ya wachezaji waliobahatika kuwa wafungaji bora kwa nyakati tofauti, Okwi amevunja rekodi za Simon Msuva na Abdulrahman Musa walioibuka wafungaji bora msimu uliopita kwa kufunga magoli 14 kila mmoja.

Okwi pia ameweza kuzivunja rekodi zilizowekwa huko nyuma na wafungaji bora kama Simon Msuva aliyewahi kufunga magoli 17, Amissi Tambwe akiwa Simba aliwahi kufunga magoli 19.

Rekodi ambayo Okwi hajaivunja ni ile ya kufunga magoli 21 ambayo yalifungwa na Tambwe akiwa Yanga, pia Okwi ana deni la kufikisha mabao 25 ya Mohamed Hussein 'Mmachinga" na Abdallah Juma aliyefunga magoli 32

Amissi Tambwe, rekodi yake ya kufunga mabao 21 iko hatarini kuvunjwa na Mganda Emmanuel Okwi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA