MBEYA CITY KUENDELEZA MOTO KWA SINGIDA UNITED LEO
Na Exipedito Mataluma. Mbeya
Baada ya kuilazimisha sare bingwa mtetezi wa Ligi Kuu bara Yanga Sc ya bao 1-1, wakusanya kodi wa jiji la Mbeya, Mbeya City inatarajia kuikaribisha Singida United katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Sokoine.
Ikumbukwe Singida United imeingia fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup na itacheza na Mtibwa Sugar Juni 2 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mjini Arusha, hivyo mchezo wa jioni ya leo utakuwa mkali na wa kusisimua, lakini wagonga nyundo hao wa jiji la Mbeya wametamba kuibuka na ushindi.
Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa mchezo kati ya Ndanda Fc na wenyeji wao Njombe Mji katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, hiyo itakuwa mechi muhimu kwa timu hizo kwani kila moja inapigania kusalia Ligi Kuu, kesho Jumamosi ligi hiyo itaendelea tena pale Turiani katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, wenyeji Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam Fc "Wanalambalamba" wa Chamazi Dar es Salaam.
Majimaji Fc itawakaribisha Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Stand United wao watawaalika majirani zao Kagera Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, lakini macho na masikio ni Jumapili katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam watani wa jadi Simba na Yanga watakapoumana