KOTEI KUIMARISHA KIUNGO SIMBA, BOCCO, OKWI KUCHAPA LAPA
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba Sc, Mfaransa, Pierre Lechantre akisaidiwa na Masoud Djuma Irambona na Mohamed Hbibi wamempanga James Kotei kusimama kama kiungo wa kati yaani namba sita huku akiendelea kuwaanzisha Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya kwenye safu ya ushambuliaji.
Mchezo huo wa Ligi Kuu bara unatazamiwa kupigwa hii leo katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam huku kila timu ikihitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika kutwaa ubingwa wa bara msimu huu wa 2017/18.
Kikosi cha Simba kimepangwa hivi
1. Aishi Manula
2. Nicolaus Gyan
3. Asante Kwasi
4. Erasto Nyoni
5. Yusuph Mlipili
6. James Kotei
7. Jonas Mkude
8. Shomari Kapombe
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Shiza Kichuya
Akiba
12. Said Mohamed
13. Poul Bukaba
14. Said Ndemla
15. Mohamed Tshabalala
16. Mzamiru Yassin
17. Laudit Mavugo
18. Rashid Juma