Yanga na Mbeya City ngoma inogile leo

Na Exipedito Mataruma. Mbeya

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga Sc jioni ya leo wanaanza kucheza viporo vyao ambapo itaumana na Mbeya City uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Yanga iliyo katika nafasi ya pili na pointi zake 47 kwa vyovyote itataka kushinda mchezo huo ili kufikisha pointi 50 na kupunguza gepu lake la pointi na mahasimu wao Simba Sc wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 59.

Lakini Simba jana imepunguzwa kasi na Lipuli Fc ya Iringa baada ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Samora mjini Iringa na kujikuta ikifikisha pointi 59 na mechi 25 wakati Yanga wao wamecheza mechi 22 tu hivyo wanaweza kuikaribia zaidi Simba iwapo watapata ushindi mechi zao tatu zilizosalia.

Yanga pia inachagizwa na ushindi wake ilioupata kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hasa baada ya kufuzu hatua ya makundi hivyo itakuwa ikisaka upya tiketi ya kushiriki tena michuano ya kimataifa mwakani

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA