Hatimaye Ally Kiba afunga ndoa na mchumba wake Mombasa

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Kiba asubuhi ya leo amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi Amina Khaleef katika msikiti uliojengwa na swahiba wake Hassan Joho ambaye ni Gavana huko Mombasa.

Taarifa ambazo zimeifikia Mambo Uwanjani, zinasema kuwa staa huyo aliwasili pamoja na familia yake tangu Jumanne iliyopita tayari kwa kushiriki shughuri hiyo kubwa leo.

Sherehe ya harusi hiyo itarushwa Live na kituo cha Azam Tv hii leo kutoka moja kwa moja kwenye ukumbi mkubwa wa kisasa wa Diamond Jubilee uliopo mjini Mombasa ambapo watu mashuhuri wanatarajia kuhudhuria akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali nchini Kenya.

Pia mwanamuziki staa Ommy Dimpoz naye ni miongoni mwa watu maarufu watakaoudhuria harusi hiyo, Ally Kiba anakuwa msanii wa kwanza nchini kufunga ndoa na kuonyeshwa live na runinga ambapo dunia itashuhudia tukio hilo

Ally Kiba na mkewe Amina Khaleef wamefunga ndoa leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA