MWANZO WA AFRIKA -3
Inaandikwa na Fikiri Salum Ilipoishia WAJERUMANI nao wakachukuwa Togoland, Cameroon na baadhi ya nchi katika Afrika ya magharibi na Afrika ya mashariki, lakini baada ya vita vya kwanza vya dunia wakanyang' anywa. Endelea Waitalia wakachukuwa Libya, Eritrea na sehemu kubwa ya Somalia. UHURU WA AFRIKA Nchi ya kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi ya Afrika Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910, Misri, katika mwaka 1922 walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tongier katika mwaka wa 1925. Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka 1956 na wakarudishiwa Tongier. Katika mwaka wa 1960:Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kongo Brazzaville, Cote D Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Nige...