Mwadui yazidi kuichimbia kaburi Mbao Fc
Na Paskal Beatus. Shinyanga
Timu ya Mwadui Fc ya mjini Shinyanga jioni ya leo imeweza kujinusuru katika janga la kutaka kushuka daraja baada ya kuilaza Mbao Fc ya Mwanza kwa bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Mwadui Complex.
Ushindi huo unawafanya Mwadui kujiweka pazuri huku kipigo hicho kikizidi kuwachimbia kaburi vijana wa Mbao Fc ambao kwa sasa wako shakani.
Goli pekee lililowapa ushindi Mwadui Fc lilifungwa na Charles Ilanfya kunako dakika ya 29 ambapo liliweza kudumu kwa dakika zote 90 za mchezo