SIMBA YAWEKA WAZI USHINDI KWAO NI LAZIMA J,PILI
Na Ikram Khamees. Morogoro
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba Sc wameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya mahasimu wao Yanga Sc utakaochezwa Jumapili uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Watani hao wa jadi wa soka la Tanzania watakutana katika mchezo wa Ligi Kuu bara huku Simba ikiwa kileleni ikifuatiwa na Yanga Sc hivyo kila moja inahitaji ushindi, Timu zote mbili zimejichimbia mjini Morogoro.
Mkuu wa kitengo cha habaro na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema ushindi kwa klabu yake ni lazima na wala hakuhitaji nguvu kuupata, amedai kikosi chao kimeimarika idara zote hivyo wanazifuata pointi zao Taifa.
Manara ameongeza kuwa msimu huu wanautaka ubingwa wa bara kwa hali yoyote ile na ili ubingwa unoge lazima umfunge Yanga