Zilizofuzu makundi kombe la Shirikisho Afrika hizi hapa
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Yanga Sc jana iliungana na timu nyingine 15 kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika na kufanya jumla ya timu 16 zitashiriki hatua hiyo.
Jumamosi majira ya saa 8;00 mchana mjini Cairo, Misri droo itachezeshwa na kutoa makundi manne ambapo kila timu itajijua kama itapangwa kucheza na timu gani, ukanda wa Afrika kaskazini ndio vinara kwa kuingia timu nyingi ikifuatiwa na Afrika magharibi, Afrika mashariki na mwisho Afrika kusini.
Timu zilizotinga hatua hiyo kutoka Kaskazini mwa Afrika ni USM Alger ya Algeria, Al Masry ya Misri, RS Berkane na Raja Casablanca za Morocco, za Afrika ya kati ni AS Vita ya DR Congo, CARA ya Congo Brazaville na El Hilal ya Sudan.
Zinazotokea Afrika mashariki ni Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda na Yanga Sc ya Tanzania, za kusini mwa Afrika ipo UD Songo ya Msumbiji, zinazotoka Afrika masharibi ni Enyimba ya Nigeria, Aduana Stars ya Ghana, Williamsville ya Ivory Coast na Djoliba ya Mali.
Yanga ilifanikiwa kukata tiketi ya kufuzu makundi jana baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Welayta Dicha na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, mabingwa hao watatua nchini leo usiku saa 7:00