KUTINYU WA SINGIDA UNITED AFUNGIWA KISA USHIRIKINA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Vitendo vya kuendekeza ushirikina vimeshamiri kwenye soka la Tanzania na safari hii limemsomba Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu anayekipiga timu ya Singida United.
Mshambuliaji huyo aliyeibuka shujaa kwa kuifungia mabao mawili muhimu dhidi ya JKT Tanzania mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mchezaji huyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi 500,000 baada ya kutupa glovu za kipa wa Mtibwa Sugar kwa mashabiki wa Singida United na kukimbia nayo.
Kitendo hicho kimesababisha kamati ya nidhamu ya TFF kumuadhibu nyota huyo ambaye amekuwa katika kiwango kikubwa, vitendo vya ushirikina vimeziponza pia timu za Mbao Fc na Simba ambazo zote zimepigwa faini ya shilingi laki tano