STAND UNITED YATISHIA KUJITOA AZAM FEDERATION CUP
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Uongozi wa timu ya Stand United "Chama la wana" ya mkoani Shinyanga, umetishia kujiondoa katika mivhuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup ikidai haijalipwa fedha zao za ushiriki tangia raundi ya kwanza hadi sasa nusu fainali.
Akizungumza leo, katibu mkuu wa klabu hiyo, Kennedy Mwangi amesema Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, halijawapa fedha zao tangu walipoanza kushiriki mivhuano hiyo na huenda wakashindwa kuingiza timu Aprili 23 mwaka huu watakapoumana na Mtibwa Sugar.
Mwangi amedai Stand United itawakaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga hatua ya nusu fainali lakini anashangaa fedha zao kuliwa na watu wa TFF, hata hivyo kuna taarifa inasema kuwa Stand United inadaiwa fedha na wachezaji wake ambao walishitaki TFF na sasa klabu hiyo inakatwa ili kufidia madeni hayo