SERENGETI BOYS YABEBA NDOO YA CHALENJI
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, maarufu Serengeti Boys jioni ya leo imefanikiwa kunyakua ubingwa wa michuano ya Cecafa- Challenge Cup baada ya kuichapa Somalia mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Burundi.
Ushindi huo wa leo ni dhahiri kwamba itawakilisha vema taifa katika fainali ya mataifa Afrika Afcon- U17 zitakazofanyika mwakani Tanzania ambapo Serengeti itakuwa mwenyeji.
Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Edson Jeremiah na Jaffari Mtoo, Serengeti ilipenya hatua ya fainali baada ya kuilaza Kenya mabao 2-1 wakati Somalia iliiondosha Uganda kwa kuichapa bao 1-0