MECHI YA LIPULI NA SIMBA YAPIGWA KALENDA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Bodi ya Ligi imeusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya wenyeji Lipuli Fc na Simba Sc uliokuwa ufanyike siku ya Ijumaa katika uwanja wa Samora mjini Iringa sasa utapigwa Jumamosi ya Aprili 21.
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema wameamua kuusogeza mbele mchezo huo kwakuwa siku ya Ijumaa wamiliki wa uwanja wa Samora wameutoa uwanja huo kwa jamii hivyo kutakuwa na shughuri nyingine.
Wambura amedai mechi hiyo itachezwa Jumamosi ikiwa ni siku moja baada ya kusogezwa mbele, tayari Simba wamesafiri leo asubuhi kuifuata Lipuli na mchezo huo inatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua, katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa Dar es Salaam