AGNES MASOGANGE AFARIKI DUNIA
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam
Video queen mwenye jina kubwa nchini, Agnes Gerald "Masogange" amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taarifa za kifo chake zimesambaa jioni hii ambapo inasemekana staa huyo amefariki katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu kufuatia kupatwa na presha ghafla.
Masogange aliyejipatia umaarufu kwa uigizaji kwenye video za wasanii wa bongofleva akitamba na msanii Belle Nine na wimbo uliojulikana sana wa Masogange, pia msanii huyo alikuwa akiandamwa na kashfa ya utumiaji dawa za kulevya na aliwahi kukamatwa nchini China, tayari mwili wake umeshapelekwa hospitali ya Muhimbili.
Mungu aiweke roho yake mahara pema peponi, Amina