Simba wazifuata pointi tatu Iringa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba Sc wameondoka leo kuelekea mjini Iringa tayari kabisa kwa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Lipuli Fc katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora Machel, Jumamosi ijayo.
Mchezo huo ulikuwa uchezwe Ijumaa ya kesho lakini kwa mujibu wa Bodi ya Ligi mchezo umesogezwa hadi keshokutwa kwa madai uwanja huo wa Samora utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.
Kikosi cha Simba ambacho kimepania kutwaa ubingwa wa bara msimu huu kimeondoka leo mapema kuifuata Lipuli, Simba iko kileleni na pointi zake 58 zikiwa ni tofauti ya pointi 11 na hasimu wake Yanga Sc ambao wanashikilia nafasi ya pili