Mtibwa Sugar na Azam Fc kumenyana leo Manungu Complex
Na Ikram Khamees. Morogoro
Moja ya mechi kali na ngumu itapigwa jioni ya leo katika uwanja wa Manungu Complex, Turiani wilayaninMvomero mkoani Morogoro wakati wenyeji Wana tamtam Mtibwa Sugar watakapoikaribisha Azam Fc wana lambalamba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Mtibwa Sugar safari hii wanaonekana kuimarika zaidi hasa kutokana na matokeo mazuri wanayoyapata karibu katika mechi zake ilizocheza hivi karibuni ikiwemo kuingia fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup.
Umahiri wa safu yake ya ushambuliaji ndiyo moja kati ya vitu vya kujivunia kwenye kikosi hicho kinachonolewa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila, lakini Azam Fc nao wamekuwa wakifanya vibaya katika mechi zake za karibuni kiasi kwamba wanaelekea kuachana na kocha wake Mromania, Aristica Cioaba.
Pia Azam Fc inakumbuka jinsi ilivyoondoshwa na Mtibwa Sugar katika michuano ya Azam Dports Federation Cup kwa mikwaju ya penalti 8-7 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana, mechi nyingine zitakazopigwa leo ni Stand United ikiwaalika jirani zao Kagera Sugar uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Majimaji Fc nayo ikiwakaribisha Ruvu Shooting uwanja wa Majimaji Songea