Wanne kutua Yanga, yumo Salamba wa Lipuli
Na Asher Maliyaga. Dar es Salaam
Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc ambao pia ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, wamejipanga kujiimarisha kwa ajili ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika na msimu ujao.
Taarifa ambazo hazina shaka kabisa zinasema mabingwa hao wamejipanga kunasa saini za wachezaji wanne ambao wataisaidia timu hiyo kwenye michuano hiyo pamoja na Ligi Kuu bara msimu ujao.
Wachezaji ambao wanatajwa kujiunga na mabingwa hao ambao huenda msimu huu wakapokwa taji lao na mahasimu wao Simba Sc ni mshambuliaji wa Lipuli Fc ya Iringa, Adam Salamba ambaye hivi karibuni alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu Bara.
Pia Yanga ina mpango wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Welayta Dicha ya Ethiopia Arafat Djako na Mnigeria Quadri Kola Aladeokun na mzawa Habibu Kiyombo wa Mbao Fc, tayari Yanga imeshapata kocha mpya Zahera Mwinyi aliyechukua nafasi ya George Lwandamina raia wa Zambia