Yanga kupaa Alhamisi kuifuata USM Alger
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Baada ya jana kuchapwa bao 1-0 na mahasimu wao wa kandanda nchini Tanzania, Simba Sc, wawakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa nchini, Yanga Sc wanatarajia kusafiri Alhamisi ijayo kuelekea mjini Algiers nchini Algeria tayari kwa mchezo wa kwanza kundi D kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga Sc itaumana na USM Alger siku ya Jumapili mjini Algiers na safari yao itaanzia Alhamisi, mabingwa hao wa bara wamepoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao hasa baada ya kuzidiwa pointi 14 na Simba wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 62 huku wao wakiwa na pointi 48 wakishikilia nafasi ya tatu.
Yanga ilifanikiwa kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho baada ya kuitoa mashindanoni Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda nyumbani 2-0 kabla ya kulala ugenini 1-0, hata hivyo Yanga imepangwa kundi moja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya