Yanga waipashia Dicha

Na Paskal Beatus. Hawassa

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc jana walianza kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha kesho Jumatano katika uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia.

Yanga ambao pia ni mabingwa wa soka nchini Tanzania, waliangukia michuano hiyo baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 na timu ya Township Rollers ya Botswana.

Katika mchezo huo utakaopigwa kesho, mabingwa hao wa Tanzania bara wanahitaji sare yoyote ama kufungwa goli moja tu ili wafuzu hatua ya makundi hasa baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 2-0 zilipokutana jijini Dar es Salaam, lakini hata hivyo Yanga itakuwa na kazi ngumu hasa baada ya kuondokewa na kocha wake mkuu, Mzambia George Lwandamina

Yanga wakipasha 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA