KUSUJUDU KWA GADIEL MICHAEL KWAZUA MSHANGAO, MWENYEWE AFAFANUA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Madhabiki wa soka nchini jana waliingia na mshangao kufuatia beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Gadiel Michael Mbaga kushangilia bao lake kwa kusujudu kama waislamu.
Beki huyo wa upande wa kulia aliyesajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam Fc, jana aliifungia Yanga bao la ushindi dhidi ya Azam Fc katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-1 na Azam Fc walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya 3 kipindi cha kwanza na Shabani Chilunda, lakini Obrey Chirwa akaisawazishia Yanga kabla ya Gadiel kufunga la pili na la ushindi.
Baada ya kufunga, Gadiel alikimbia pembeni na kuinama chini akiswali kwa mtindo wa kusujudu ambao unatumiwa sana na waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya kufanya hivyo mashabiki wa soka walishangazwa huku wengine wakidai mchezaji huyo ni Muislamu na wengine wakidai hata Wakristo hufanya hivyo.
Lakini baadaye Gadiel alitolea ufafanuzi kuwa aliamua kusujudu akiwasalimia viongozi wa Azam Fc ambao alifanya nao kazi vizuri lakini walimzuia asijiunge na Yanga na walitaka akae nje mpaka mkataba wake uishe hivyo amewaonyesha kitu kwa kufunga bao la kistadi