YANGA YAWASHA ENDIKETA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc jioni ya leo imewasha endiketa zake baada ya kuilaza Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa uahindi huo Yanga imekwea kutoka nafasi ya tano hadi ya tatu ikifikisha pointi 25 sawa na Mtibwa Sugar lakini ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga, Yanga imecheza mechi 13 na iliingia uwanjani leo ikisaka ushindi kwa udi na uvumba.

Goli ambalo limeipa ushindi Yanga limefungwa na mshambuliaji wake chipukizi Pius Buswita aliyepokea pasi ya Ibrahim Ajibu, hadi timu hizo zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo, timu zote zilishambuliana kwa zamu hadi mwisho matokeo ndiyo hayo

Pius Buswita ameifungia Yanga bao pekee

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA