Azam Fc yawalambisha Ice Cream tano Shupavu Fc
Na Mwandishi Wetu. Morogoro
Klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam Fc mchana wa leo imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuilaza timu ya Shupavu mabao 5-0 uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Huo ni ushindi mkubwa kwa vijana hao wa Said Salim Awadh Bakhresa ambao Jumamosi iliyopita walifungwa mabao 2-1 na Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Azam ilijipatia mabao mawili kipindi cha kwanza moja likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Yahaya Zayd kabla ya Iddi Kipagwile, magoli mengine matatu yamefungwa na Paul Peter na kuwa hat trick yake ya kwanza kwenye michuano hiyo