KAGERA SUGAR VS SIMBA NI MECHI YA KISASI
Na Paskal Beatus. Bukoba
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa kuzikutanisha Kagera Sugar na Simba Sc katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Huo ni mchezo wa kisasi kutokana na kumbukumbu ya msimu uliopita ambapo Simba ililala 2-1 mpaka kuamua kukata rufaa TFF kisha kutishia kwenda Fifa kwa kile kilichodaiwa Kagera Sugar kumchezesha Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Kwa maana hiyo mechi ya leo itakuwa ya kisasi, Simba ikitaka kulipiza kisasi, lakini pia itakuwa mechi ya uhasama kwani inawakutanisha tena Juma Nyosso na John Bocco ambao walikuwa maadui hawapatani na hasa Nyosso alimtomasa makalioni Bocco hivyo hatujui leo kitatokea kitu gani Kaitaba, Simba ikishinda ama kutoka sare itarejea kileleni