Sibuka sasa kutangaza live Ligi Kuu England
Na Alex Jonathan. Dar es Salaam
Kituo cha redio Sibuka cha jijini Dar es Salaam kimeanza kutangaza mechi za Ligi Kuu ya England (EPL) na kuwataka wapenzi wa soka kujitokeza kusikiliza kwani wanaweza kuibuka mamilionea.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, mtangazaji wa redio hiyo David Pasko (Pichani) amesema kituo chake kimeanza kutangaza live ligi ya EPL.
Amedai Watanzania wamekuwa wakipenda kufuatilia ligi ya England hivyo wameamua kuwaletea matangazo hayo moja kwa moja, pia Pasko amesema kituo chake kitaendelea kurusha matangazo ya moja moja ya mpira wa Ligi Kuu Bara