Nyosso ashikiliwa na polisi kwa kumpiga shabiki wa Simba
Na Paskal Beatus. Bukoba
Beki wa Kagera Sugar, Juma Said Nyoso anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Kagera baada ya kudaiwa kumpiga shabiki wa Simba anayesemakana kumdhihaki mchezaji huyo.
Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo kwa sasa, zinasema kuwa Nyoso alitaka kumchapa Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara lakini polisi waliingilia kati na kuwanusuru wawili hao.
Lakini Nyoso akiwa anaelekea kwenye gari la timu yake ya Kagera Sugar akakutana na shabiki wa Simba aliyemshambulia mchezaji huyo ndipo alipoamua kumdunda shabiki huyo na kumuumiza vibaya.
Shabiki huyo amekimbizwa hospitalini na mchezaji huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi