NINJE AMPONZA MAYANGA STARS
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) limetangaza kuanzisha mchakato wa kusaka kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars akichukua mikoba ya Salum Mayanga anayemaliza mkataba wake.
Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka ni kwamba mkataba wa Mayanga upo ukingoni na mipango ya TFF kwa sasa ni kuajili kocha mzungu.
Lakini inasemekana kuwa kufanya vibaya kwa Tanzania Bara katika michuano ya Chalenji iliyofanyika Kenya ambapo karibu kikosi chote cha Bara ni kilekile cha Mayanga na hivyo kimepelekea Watanzania kutokuwa na imani naye.
Bara ilikuwa ikinolewa na Ammy Ninje, ambaye pia alikuwa msaidizi wa Mayanga kwenye kikosi cha Stars, kwa mujibu wa TFF mchakato wa kusaka kocha mpya walimu kutoka Zanzibar nao wametakiwa kutuma maombi