Yanga na Ruvu Shooting ni machozi jasho na damu
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kinaendelea tena leo kwa viwanja vitatu nyasi kuwaka moto, kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mabingwa watetezi Yanga Sc watakuwa wageni wa Ruvu Shooting ya Pwani.
Huo ni mchezo mwingine kwa Yanga ambao wapo katika wakati mgumu kwa sasa hasa baada ya kuandamwa na majeruhi na nyota wake wa kikosi cha kwanza, hata hivyo wamejinasibu kushinda mchezo huo ingawa Ruvu Shooting nao si wa kubeza.
Mechi nyingine leo zitapigwa mikoani, Tanzania Prisons itawaalika Azam Fc uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Mwadui Fc wataikaribisha Ndanda pale Mwadui Complex Shinyanga