AZAM FC YAMSHITUKIA NKONGO
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Uongozi wa klabu bingwa ya soka Afrika mashariki, Azam Fc wameiandikia barua Bodi ya Ligi (TPLB) likimpinga mwamuzi wa kati Israel Nkongo.
Nkongo atachezesha mechi yao dhidi ya mabingwa watetezo Yanga Sc itakayopigwa kesho mishale ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Katika madai yao Azam kwa TPLB wanataka mwamuzi huyo abadilishwe kwakuwa anapopewa dhamana ya kuchezesha mechi zao zimekuwa na malalamiko, Azam wanathibitisha kuwa Nkongo hafai kuchezesha pambano lao na Yanga kwani amewahi kushindwa mara kadhaa kwenye mechi zao.
Mwamuzi huyo aliwahi kuchezesha mechi ya Yanga na Azam na Azam kushinda mabao 3-0 na wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Stephano Mwasika walimshambulia mwamuzi huyo, hivyo hawataki yatokee hayo hiyo kesho