Mashabiki Yanga wamkumbuka Mwambusi
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kufuatia kiwango kibovu inachokionyesha Yanga kwa sasa, baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wamemkumbuka aliyekuwa kocha msaidizi Juma Mwambusi wakidai ni bora yeye kuliko Shadrack Nsajigwa.
Wakizungumza tofauti kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki hao wameelezea hisia zao na kudai kwa sasa Yanga haiwapi raha kwani soka wanalocheza haliwavutii na timu yao inazidi kuwapa presha.
Wanadai Yanga inacheza soka ambalo hawajazoea kuliona kwani hata ushindi wake umekuwa wa bahati, Yanga iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini Ruvu ndio waliutawala mchezo huo.
Hivyo wameutaka uongozi wa Yanga kumrejesha haraka kocha msaidizi Juma Mwambusi ambaye amejiuzuru ili aweze kuinusuru timu yao, kwani Mwambusi amefanya vizuri alipohudumu kwenye nafasi hiyo