Simba yaihofia Azam, yataka mechi yake isogezwe mbele

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc imeanza kuingia mchecheto baada ya kuitaka Bodi ya Ligi (TPLB) kuisogeza mbele mechi yake dhidi ya Azam Sc itakayochezwa Februali 11 mwaka huu.

Akizungumza jana, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara amesema ratiba yao inawapa ugumu kidogo kwani kwa sasa akili zao wanazielekeza kwenye michuano ya kimataifa ambapo Simba itacheza na Wadjibout.

Manara amedai ratiba ya Ligi Kuu Bara inawabana kwani Simba itacheza na Ruvu Shooting Februali 4 kisha na Azam Fc halafu itaenda Shinyanga kucheza na Mwadui kabla ya kucheza kombe la Shirikisho barani Afrika.

Manara amedai mipango ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na ndio maana wamemchukua kocha Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye amewahi kuipa ubingwa wa Afcon, Cameroon mwaka 2000.

Kwa maelezo ya Manara, Simba wanaiomba Bodi ya Ligi iwasogezee mbele mchezo wao dhidi ya Azam ikiamini itajipanga vizuri, lakini ni sawa kama inaigwaya kwani timu hizo zilipokutana hivi karibuni katika michuano ya kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, Simba ilifungwa bao 1-0 hivyo imeingia hofu

Haji Manara Afisa habari wa Simba Sc

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA