Yanga na Azam hapatoshi Chamazi
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam litasimama kwa muda kupisha vita ya mafahari wawili mabingwa wa kombe la Kagame Azam Fc na mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Sc katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Azam Fc ikicheza nyumbani ina kila sababu ya kuweza kuzoa pointi tatu na kukaa kileleni ikiishusha Simba inayoongoza kwa sasa ikiwa na pointi 32, Azam yenyewe ina pointi 30 lakini ikishinda itafikisha pointi 33.
Kwa upande wa Yanga watakaocheza bila makocha wao George Lwandamina na Shadrack Nsajigwa, pia ikiwakosa nyota wake wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi, ila Obrey Chirwa ataiongoza safu ya ushambuliaji akishirikiana na Ibrahim Ajibu na Raphael Daudi.
Azam Fc wao wako kamili wakiwa na nyota wao Himid Mao, Salum Abubakar, Frank Domayo, Benard Athur, Iddy Kipagwile na wengineo bila shaka mchezo utakuwa mkali.
Mechi nyingine za ligi hiyo zitapigwa leo ambapo pale Sokoine Mbeya, wenyeji Mbeya City watawaalika Mtibwa Sugar, kule Mwadui Complex Shinyanga, wenyeji Mwadui Fc wataialika Njombe Mji na pale Kaitaba mjini Bukoba, Kagera Sugar watakipiga na Lipuli Fc