AZAM FC YAISHUSHA SIMBA KILELENI

Na Exipeditor Mataruma. Mbeya

Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc jioni ya leo imeifunga Tanzania Prisons mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ikicheza nyumbani, Prisons waliweza kuibana Azam Fc kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi ya kushutukiza, lakini hadi mapumziko timu zote zilienda zikiwa hazijafungana hata bao.

Kipindi cha pili dakika ya 77 Azam walijipatia bao la kuongoza likifungwa na kinda Yahya Zayd kabla ya dakika ya 83 kinda mwingine Paul Peter kufunga la ushindi, kwa matokeo hayo Azam wanakamata usukani wakifikisha pointi 30 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 29.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara timu ya Mwadui ililazimishwa sare ya  1-1 na Ndanda Fc uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa Simba Sc na Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba na Majimaji na Singida United kule Songea

Azam imeidunga Prisons 2-0 leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA