KOCHA WA SIMBA B ACHEKELEA KUIPANDISHA FRIENDS RANGERS
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Kocha wa zamani wa kikosi cha Simba B, Said Msasu "Nagri" ameanza kuchekelea kikosi chake cha sasa cha Friends Rangers ya Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam kuelekea kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Msasu ambaye amewahi pia kuzichezea Simba Sc, Lipuli Fc na Singida United amedai timu yake ya Friends Rangers itapanda Ligi Kuu Bara licha kwamba bado wana mchezo mkononi dhidi ya JKT Mgambo.
Friends ipo kundi C ambalo tayari timu ya JKT Ruvu imeshapanda Ligi Kuu na ushindani sasa upo kwao na African Lyon, Friends Rangers ina pointi 22 wakati Lyon ina pointi 21 na zote zimecheza mechi 12 hivyo ana uhakika kabisa ya kuipandisha Ligi Kuu timu hiyo iliyosotea nafasi kwa misimu kadhaa