Diamond Platinum atembelea yatima Rwanda
#BURUDANI: DIAMOND PLATINUM ATEMBELEA YATIMA RWANDA.
Msanii wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, bongofleva, Nasibu Abdul au Diamond Platinum ametembelea kituo cha watoto yatima nchini Rwanda na kutoa misaada mbalimbali.
Mwanamuziki huyo aliamua kutua Rwanda baada ya safari zake za kimuziki ikiwemo kufuata tuzo yake aliyoshinda nchini Nigeria.
Msanii huyo amekuwa akijitolea na kusaidia makundi mbalimbali ya wasiojiweza wakiwemo watoto, tayari msanii huyo anamiliki kundi kubwa la muziki WCB lililokusanya wasanii mbalimbali na ametambulisha biashara yake ya karanga zilizowapa ajira vijana wa Afrika mashariki