Simba na Majimaji ngoma inogile Taifa leo
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc jioni ya leo inaumana na Majimaji ya Songea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni muendelezo wa Ligi Kuu Bara kukamilisha mzunguko wa kwanza, Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 32 ikifuatiwa na Azam yenye alama 30 na Yanga ikikamata nafasi ya tatu ikiwa na alama 28.
Majimaji imekuwa ngumu kufungwa na vigogo msimu huu hasa ikicheza uwanja wake wa nyumbani Majimaji Stadium mjini Songea kwani iliweza kuzibana, Yanga Sc, Azam Fc na Singida United, na kwa mujibu wa kocha wao mkuu Habibu Kondo amesema hata Simba wataibania leo.
Timu hiyo inajivunia safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Peter Mapunda, Marcel Boniventure, Seleman Kassim Selembe na Jerryson John wakati Simba yenyewe inatambia nyota wake Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, John Bocco na Jonas Mkude, mchezo mwingine utapigwa mjini Mbeya wakati wenyeji Tanzania Prisons wakiialika Singida United