Stand United yaikatakata Mbao Fc CCM Kirumba
Na Paskal Beatus. Mwanza
Timu ya Stand United ya mjini Shinyanga, jioni ya leo imeitoa nishai Mbao Fc baada ya kuichapa bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba jijini Mwanza, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa ushindi huo moja kwa moja Stand United imekwea hadi nafasi ya 11 ikifikisha pointi 14, goli pekee lililoipa ushindi Stand United limefungwa kwa mkwaju wa penalti kunako dakika ya 40 na Vitalis Mayanga.
Penalti hiyo ilisababishwa na kipa wa Mbao Fc, Ivan Rugumandiye ambaye alimkamata miguu mshambuliaji wa Stand United, Landry Ndikumana na wote kuanguka wakiwania mpira kwenye box, Mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara ulifanyika katika uwanja wa Manungu Complex Morogoro ambapo Mtibwa Sugar ilitoka suluhu 0-0 na Njombe Mji