SIMBA SIYO YA MCHEZO MCHEZO, YAIFANYIA KITU MBAYA MAJIMAJI

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Simba Sc imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya jioni ya leo kuifanyia kitu mbaya Majimaji ya Songea kwa kuifunga mabao 4-0 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ilishuhudiwa Simba ikiongoza kwa mabao mawili hadi ingwe ya kwanza inamalizika kwa magoli yaliyofungwa na nahodha John Raphael Bocco.

Kipindi cha pili Emmanuel Okwi akaongeza mengine mawili na kufanya Simba iibuke na ushindi mnono wa 4-0 na kuendelea kuchanua kileleni.

Huo ni ushindi wa kwanza wa kocha Mfaransa, Pierre Lechantre aliyechukua mikoba ya Joseph Omog raia wa Cameroon, kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 35 na mechi 15 ikizidi kuiacha Azam Fc kwa zaidi ya pointi 5

Emmanuel Okwi (wa kwanza kulia) akishangilia sambamba na Said Ndemla

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA