NDANDA FC YAIZAMISHA STAND UNITED

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Timu ya Ndanda Fc "Wanakuchele" jioni ya leo imeizamisha Stand United bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Matokeo hayo yanaifanya Ndanda Fc kuchupa hadi nafasi ya saba ikiwa na pointi 16 katika mechi 14 ilizocheza.

Bao pekee lililoipa ushindi Ndanda inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Mlandege, Malale Hamsini lilifungwa na straika wake matata Omari Mponda, Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi mbili kupigwa, Ruvu Shooting na Mbao Fc uwanja wa Mabatini Mlandizi, Mwadui Fc na Njombe Mji uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga

Ndanda Fc imeifunga Stand United leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA