Bocco, Ndemla wairejesha Simba kileleni
Na Paskal Beatus. Bukoba
Simba Sc imerejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya jioni ya leo kuilaza Kagera Sugar kwa mabao 2-0 uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Iliwachukua kipindi cha pili Simba kujipatia mabao hayo baada ya kucheza dakika 45 za mwanzo bila kufungana, Kagera Sugar walionekana kuimudu Simba baada ya kuizuia isipate bao hadi zilipoenda kupumzika.
Kipindi cha pili Simba ilirejea uwanjani ikiwa na kasi mpya na kuanza kujipatia mabao yake yaliyoipa pointi tatu na kuishusha kileleni Azam Fc iliyokamata kiti hicho kwa muda, mabao ya Simba yamefungwa na Said Ndemla na John Bocco "Adebayor", kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 32 ikicheza mechi 13 na mwishoni mwa wiki itaumana na Majimaji