MBAO FC KAZI WANAYO LEO KWA RUVU SHOOTING MABATINI
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena hii leo kwa mitanange miwili kupigwa katika viwanja tofauti, lakini mechi ambayo ni gumzo itapigwa Mlandizi.
Ruvu Shooting iliyofanyiwa marekebisho kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kukosa mabao mengi ya wazi dhidi ya Yanga Sc, itawakaribisha Mbao Fc ya Mwanza katika uwanja wake wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire leo Mbao Fc kazi wanayo kwani wamewaandalia misumeno ya kufa mtu kwa ajili ya kuikatakata jioni ya leo, mchezo mwingine utapigwa Mwadui Complex kati ya wenyeji Mwadui Fc na Njombe Mji