Ruvu Shooting yainyoosha Mbao
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Masarange wa Ruvu Shooting ya Mlandizi Kibaha mkoani Pwani jioni ya leo imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini baada ya kuilaza Mbao Fc mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa ushindi huo Ruvu Shooting imefikisha pointi 14 na sasa imetoka mkiani nafasi ya 16 na kupanda hadi ya 11, Ruvu Shooting waliupania vilivyo mchezo huo hasa wakikumbuka kichapi walichokipata msimu uliopita kutoka kwa Mbao cha mabao 4-0.
Hivyo leo wamelipiza kisasi kwa ushindi huo, mabao yote ya Ruvu Shootibg yamefungwa na Mcha Khamis, ligi hiyo itaendelea tena kesho viwanja vinne vikiwaka moto, Azam Fc vs Yanga, Mwadui Fc vs Njombe Mji, Mbeya City vs Mtibwa Sugar na Kagera Sugar vs Lipuli Fc