Singida United yashikwa shati Songea
Na Mwandishi Wetu. Songea
Timu ya Majimaji Fc ya Songea jioni ya leo imeibana mbavu Singida United baada ya kwenda nayo sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Kwa matokeo hayo Singida United imeshindwa kuchupa kutoka nafasi ya tano waliyopo sasa hadi ya tatu endapo wangepata ushindi dhidi ya Majimaji, katika mchezo huo wa leo Singida United walitangulia kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 28 kipindi cha kwanza na Papy Kambale.
Lakini vijana wa Majimaji waliweza kujitutumua na kuweza kusawazisha bao hilo lililowapa pointi moja muhimu lilifungwa na mshambuliaji wake Peter Mapunda kunako dakika ya 83, Singida United bado wana kumbukumbu mbaya ya kuchapwa mabao 4-0 na Simba Sc