Shamte atambia Halima wake

Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Msanii anayechipukia wa muziki wa kizazi kipya maarufu Bongofleva, Shukuru Nassoro "Shamte" ametamba kufanya vizuri na wimbo wake mpya "Halima" ambao tayari ameshautambulisha kwenye Media.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Shamte amesema tayari wimbo wake ameshausambaza kwenye mitandao ya kijamii na amedai wimbo huo utamtoa kimuziki.
Akielezea mahadhi aliyotumia katika wimbo huo alionshirikisha nyota wa muziki wa Singeli Side Kichwa amedai ametumia miondoko ya Singeli.
Ameongeza kuwa Halima ni hadithi ya kweli kabisa na ameamua kufikisha ujumbe, wimbo huo umeanza kupa viewers wengi kwenye mtandao wa youtube na amewataka mashabiki wake kuuchangamkia ili kumpa nguvu ya kuachia ngoma nyingine, msanii huyo kwa sasa anaishi Temeke Dar es Salaam

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA