SINGIDA UNITED YAWANG' OA WABABE WA SIMBA USIKU HUU
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Timu ya Singida United imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA baada ya kuifunga timu ya Green Warriors mabao 4-3 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penalti baada ya sare tasa 0-0 ndani ya dakika 90.
Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi usiku huu na kuifanya timu hiyo inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm kusonga mbele hatua ya 16 bora.
Mbali na Singida United kutinga hatua ya 16 bora, timu ya Mtibwa Sugar nayo ilitinga hatua kama hiyo baada ya kuilaza Majimaji Rangers mabao 2-1 uwanja wa Ilulu mjini Lindi huku mabao yote ya washindi yakifungwa na Kevin Sabato "Kiduku".
Matokeo mengine kama ifuatavyo Tanzania Prisons 5 Burkina Faso 4 (Penalti) baada ya sare 1-1, Sokoine Mbeya, Majimaji Songea 2 Ruvu Shooting1, Majimaji Stadium, Songea, Njombe Mji 4 Rhino Rangers 1 (Penalti) baada ya sare ya 2-2, Sabasaba Stadium, Njombe.
Matokeo mengine ni Stand United 2 Pamba Fc 0, CCM Kirumba, Mwanza, Kiluvya United 2 JKT Oljoro 0, Mabatini, Mlandizi Pwani na mechi kati ya KMC na Toto Africans imesogezwa mbele hadi Februali 7 mwaka huu