JPM NA MKEWE WACHANGIA SHILINGI MILIONI 15 KWA WASTARA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamemchangia shilingi milioni 15 msanii wa filamu nchini Wastara Juma ili arudi hospitali ya Sifael nchini India, kwaajili matibabu chini ya uangalizi wa hospital hiyo.
Fedha hizo zimekabidhiwa kwake na katibu wa Rais Ngusa Samike ambaye pia amemkabidhi Wastara shilingi milioni moja na laki tisa zilizochangwa na wasaidizi wa Rais, makabidhiano yakifanyika nyumbani kwa Wastara, Tabata Dar es Salaam.
Hivi karibuni msanii huyo alikuwa akiomba msaada wa pesa kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili arudi hospitali na kufikia hatua ya kuandika na kusambaza mtandaoni waraka maalum kwa Rais Magufuli, akiomba msaada.