JULIO ACHEKELEA KUIADHIBU MWADUI FC
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kocha wa Dodoma Fc ya mkoani Dodoma, Jamhuri Kihwelu "Julio" amechekelea ushindi wa timu yake dhidi ya Mwadui Fc wa mabao 2-1 jana katika uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo, Julio amesema amejisikia furaha kuifunga Mwadui kwani ni timu yake ya zamani ambayo aliwahi kuipandisha Ligi Kuu Bara hivyo anayajua mapungufu ya timu hiyo.
Dodoma Fc inayopigania kupanda Ligi Kuu Bara, jana ilifanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA kwa kuilaza Mwadui 2-1, hata hivyo Julio amekisifu kikosi cha Mwadui kuwa kimecheza vizuri na kuipa ushindani Dodoma Fc