Cannavaro asema vijana wanaiangusha Yanga
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Beki na nahodha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc, Nadir Haroub Ally "Cannavaro" amesema wachezaji vijana wanaiangusha Yanga na ndio maana hawatishi msimu huu.
Akizungumza na gazeti moja la michezo linalotoka kila siku, Cannavaro amesema uwepo wa wachezaji wengi vijana kwenye kikosi hicho kwa sasa hakiwapi matokeo ya kuridhisha mashabiki wa Yanga tofauti na wao walivyokuwa wakiaminiwa.
Amedai kukosekana kwa mastaa kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na wengineo kunawanyima matokeo na soka la kuvutia, beki huyo amedai vijana hawajitumi ingawa kwa sasa hawana jinsi.
"Mpango wa Yanga kwa sasa ni kukaa na vijana na sababu kubwa vijana hawa watakuja kuwa mastaa hapo baadaye lakini tatizo lao hawajitumi ipasavyo, Yanga ni jina kubwa na ina mashabiki wengi na wanataka matokeo na soka la kuridhisha, lakini vijana wanajitahidi ila hawajitumi", alisema nahodha mwenye heshima kubwa katika klabu hiyo