YANGA TIA MAJI TIA MAJI YATINGA 16 BORA YA FA CUP
Na Exipedito Mataruma. Mbeya
Mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu FA Cup baada ya jioni ya leo kuiondosha Ihefu Fc kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, iliwabidi Yanga wasubiri hadi dakika ya 90 ya mchezo kusawazisha bao kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Obrey Chirwa.
Mwamuzi Athuman Razi wa Morogoro aliipa Yanga penalti baada ya Obrey Chirwa kukwatuliwa na beki wa Ihefu ndani ya box, Ihefu walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha kwanza dakika ya 36 kufuatia beki wa Yanga, Andrew Vicent "Dante" kujifunga.
Katika mikwaju ya penalti Yanga walipata nne zilizopigwa na Kevin Yondan, Hassan Kessy, Gadiel Michael na Raphael Daudi, wakati Papy Kabamba Tshishimbi na Obrey Chirwa walikosa.
Penalti za Ihefu zilifungwa na Andrew Kayuni, Mhando Mkumbwa, na Jonathan wakati Abubakar Kidungwe, Emmanuel Mamba na Richard Ng' ondya walikosa.
Makipa wa timu zote, Yanga Youthe Rostand na Andrew Kayuni wa Ihefu walikuwa nyota kwa timu zao, Kayuni akiisaidia Ihefu ndani ya dakika 90 wakati Rostand akiisaidia Yanga kwenye mikwaju ya penalti