KOCHA WA MWADUI AFARIKI DUNIA
Na Mwandishi Wetu. Shinyanga
Kocha msaidizi wa timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga, Jumanne Ntambi amefariki dunia usiku huu baada ya kuanguka bafuni wakati akioga.
Kocha huyo ameanguka na kufariki papo hapo licha ya jitihada za kumwahisha hospitali zilipofanywa lakini madaktari wakathibitisha Ntambi kupatwa na mauti.
Ntambi alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipewa likizo ingawa jana alienda kuwajulia hali wachezaji wake. Mungu ailaze mahara pema peponi, Amina